Laptop ya kwanza yenye skrini tatu yazinduliwa Marekani | TRICKS ZOTE

Laptop ya kwanza yenye skrini tatu yazinduliwa Marekani

 Kampuni inayotayarisha michezo ya kompyuta ya Razer imezindua kipakatalishi (kompyuta ya kupakata/laptop) mpya ambayo ina skrini tatu kwe...

 Kampuni inayotayarisha michezo ya kompyuta ya Razer imezindua kipakatalishi (kompyuta ya kupakata/laptop) mpya ambayo ina skrini tatu kwenye maonyesho ya teknolojia mpya mjini Las Vegas.

Kampuni hiyo imesema laptop hiyo ambayo imeundwa kupitia mradi uliopewa jina Valerie, ndiyo ya kwanza ya aina yake duniani.

Skrini zote tatu ni za kiwango cha kuonyesha pikzeli 4,000 (4k).
Zote ni za ukubwa wa inchi 17 (43cm). Skrini mbili huchomoza kila upande kutoka kwa skrini kubwa ya kati, moja kwa moja.
 Mmoja wa wachanganuzi wa teknolojia mpya amesifu sana laptop hiyo na kusema wachezaji wa michezo ya kompyuta siku hizi wamekuwa wakitafuta kompyuta za kisasa zaidi, ghali na zenye uwezo wa kipekee. Kompyuta hiyo inapozimwa na kufungwa, ina upana wa inchi 1.5.

Razer wamesema inalingana na laptop nyingi sana zinazotumiwa kwenye michezo ya kompyuta, ambao kawaida huwa kubwa kidogo kuliko kompyuta zinazotumiwa nyumbani na ofisini.

"Tulifikiria, 'Huu ni kama wendawazimu, tunaweza kufanya hivi," msemaji wa kampuni hiyo aliambia BBC.
"Jibu lilikuwa: 'Naam, tuna kichaa vya kutosha, tunaweza'."

Laptop iliyozinduliwa ni ya maonesho tu na Razer hawajasema ni lini wataanza kuunda kompyuta kama hizo za kuuza.

Project Valerie ni moja tu ya laptop za michezo ya kompyuta zilizozinduliwa kwenye maonesho ya CES.

Acer walizindua laptop kubwa ya inchi 21 ambayo inaitwa Predator 21X, ambayo inagharimu $8,999 (£7,250).
Samsung nao wamezindua laptop yao ya kwanza ya michezo iitwayo Samsung Notebook Odyssey, ambazo ni za ukubwa mara mbili - za inchi 17 na za inchi 15.

COMMENTS

Name

Adsense,4,Advertise,1,Android,14,Antivirus,6,Apple,2,Apps,1,Blog / Magazine,1,Blog /Magazine,1,Blogger,1,Blogger Template,5,Blogging,5,Business,3,CodeCanyon,2,Computer,3,Corporate,3,Earn Money,1,Facebook,2,Gadget,2,Games,1,Gbwhatsapp,1,Hack,1,Hacker,1,Hp,1,Htc,1,HTC One M9,1,Huawei,1,Instagram,5,Internet,2,iOS,3,iPhone,1,iThemes,1,Laptop,1,Lenovo,1,MacBook,1,Magazine,1,Microsoft Surface Book,1,Mobile,9,Modem,4,News,9,News & Magazine,1,Nonprofit,1,Operating Systems,3,Personal,1,Personal Blogger Template,1,Phones & Tablets,8,Plugins,3,Premium Blogger Template,5,Responsive blogger templates,4,Review,2,Root,2,Samsung,1,Security,1,Seebait,1,Seo,3,Serial key,5,Software,1,Softwares,2,Solutions,3,Sony,2,Tablets,1,Tecno,2,Telegram,1,ThemeForest,9,Tigo,1,Top 10,1,Tricks,7,Tricks And Tips,13,Tutorial,41,Ubuntu,2,Unlock,3,Utilities,1,Video,1,Videos,1,Vodacom,1,Webdesigns,1,Whatsapp,14,Window7,2,Window8,1,Windows,4,Windows 10,2,Windows 7,3,Windows 8,2,Windows 8.1,1,WordPress Themes,7,WordPress Tutorials,1,Youtube,3,
ltr
item
TRICKS ZOTE: Laptop ya kwanza yenye skrini tatu yazinduliwa Marekani
Laptop ya kwanza yenye skrini tatu yazinduliwa Marekani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrEhMdl17i_ik5azIdvxBZceeey_X-ahAkShcdFSA5jbXzfgrG3TS9m1ZpZXkvIUpXiXqQP_Djkaepd73StDd6pZRrsCM-ESVJHqSayn6C2f0_ZlHghqdGzsUrQrF_lS6YpCt6ys9NNEw/s1600/_93284739_razer-1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjrEhMdl17i_ik5azIdvxBZceeey_X-ahAkShcdFSA5jbXzfgrG3TS9m1ZpZXkvIUpXiXqQP_Djkaepd73StDd6pZRrsCM-ESVJHqSayn6C2f0_ZlHghqdGzsUrQrF_lS6YpCt6ys9NNEw/s72-c/_93284739_razer-1.jpg
TRICKS ZOTE
http://zotekalitricks.blogspot.com/2017/01/laptop-ya-kwanza-yenye-skrini-tatu.html
http://zotekalitricks.blogspot.com/
http://zotekalitricks.blogspot.com/
http://zotekalitricks.blogspot.com/2017/01/laptop-ya-kwanza-yenye-skrini-tatu.html
true
1497846088060985027
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy