JINSI YA KUBURN UBUNTU AU WINDOWS KWENYE FLASH DISK | TRICKS ZOTE

JINSI YA KUBURN UBUNTU AU WINDOWS KWENYE FLASH DISK

Katika tutorial hii nitawaonyesha jinsi ya kuburn ubuntu kwenye flash disk. Kwa kawaida watu wengi huwa wanainstall operating systems kwa ku...

Katika tutorial hii nitawaonyesha jinsi ya kuburn ubuntu kwenye flash disk. Kwa kawaida watu wengi huwa wanainstall operating systems kwa kutumia CD au DVD kwa sababu tu ndo njia ambayo imekuwa ikitumika kwa muda mrefu. Ukweli ni kwamba kuinstall kwa kutumia flash disk kunachukua mda mfupi zaidi kuliko CD au DVD.Sababu ni kwamba kompyuta ikihitaji data, CD inabidi izunguke mpaka ifike mahali ambapo ile data ipo ndo kompyuta iisome, wakati kwa flash disk hakuna kuzunguka, data inapatikana hapo hapo. Ntawaonyesha njia mbili, moja kuburn ukiwa kwenye ubuntu na nyingine kuburn ukiwa kwenye windows. Kabla hujaendelea download file la ubuntu hapa au kwenya links chini kabisa mwisho wa hii tutorial. Au kama unalo tayari unaweza kuendelea.

Kuburn ukiwa kwenye ubuntu

Kama unatumia ubuntu tayari au kuna rafiki yako ana ubuntu basi hii ndo njia rahisi kabisa ya kuburn ubuntu kwenye flash disk. Ubuntu huwa inakuja ikiwa na program inayoitwa "Startup Disk Creator", unaweza kutumia hii program kuburn ubuntu kwenda kwenye flash disk. Kwa wanaotumia ubuntu kuanzia version 11.04 kwenda juu watabonyeza start menu, kile kitufe cha kwenye kona kabisa, kisha search kwa kuandika "startup disk creator", ikitokea ibonyeze.
Kwa wanaotumia ubuntu version 10.04 kwenda chini, bonyeza System-->Administration-->Startup Disk Creator

Program ikishafunguka bonyeza "Other" ili kuonyesha setup file lako la ubuntu lilipo. 


Chagua hilo file na bonyeza "Open"

 Mahali palipo andikwa "Disk to use" chagua flash disk unayotaka kuitumia, zitatokea nyingi kama utakuwa umechomeka flash disk zaidi ya moja. Kisha bonyeza "Make Startup Disk".
 Kompyuta itaanza kucopy mafile kwenda kwenye flash disk, inaweza ikataka uweke password yako ya ubuntu wakati inaendelea, weka password, Ikishamaliza flash disk yako ipo tayari kutumika!

Kuburn ukiwa kwenye windows

Window haiji na program kwa ajili ya kuburn operating systems to ubuntu, hivyo basi inabidi udownload UNetbootin kutoka hapa. Hakikisha flash disk yako imeformatiwa kwa FAT32 au FAT16 format, kwa kuright-click kisha format, halafu chagua FAT32 au FAT16. Kabla hujaformat copy vitu vyako mahali pengine. Kisha bonyeza UNetbootin uliyoidownload, bonyeza yes kwenye window itakayotokea. 

Kisha chagua mahali palipoandikwa "Diskimage", kisha bonyeza "..." ili kuchagua setup file lako la ubuntu lilipo, usichague "Distribution" hiyo imewekwa kama haujadownload ubuntu tayari, itadownload ubuntu na itaiburn kwenye flash disk.Ukishachagua setup file bonyeza "Open".

 Chagua flash disk unayotaka kutumia kuburn ubuntu, kisha bonyeza "OK".
 Kompyuta itaanza kucopy mafile, subiri kidogo ikishamaliza, flash disk yako ipo tayari kutumika!
"This program installed correctly"

 Ikishamaliza unaweza ukachagua kureboot moja kwa moja, au ukaexit na kureboot baadae muda utakao amua.
 Ukishamaliza windows inaweza kukupa warnings kwamba program(UNetbootin) haikuinstall vizuri, ziignore kwa sababu UNetbootin haihitaji kuinstaliwa. Chagua "This program installed correctly".

COMMENTS

Name

Adsense,4,Advertise,1,Android,14,Antivirus,6,Apple,2,Apps,1,Blog / Magazine,1,Blog /Magazine,1,Blogger,1,Blogger Template,5,Blogging,5,Business,3,CodeCanyon,2,Computer,3,Corporate,3,Earn Money,1,Facebook,2,Gadget,2,Games,1,Gbwhatsapp,1,Hack,1,Hacker,1,Hp,1,Htc,1,HTC One M9,1,Huawei,1,Instagram,5,Internet,2,iOS,3,iPhone,1,iThemes,1,Laptop,1,Lenovo,1,MacBook,1,Magazine,1,Microsoft Surface Book,1,Mobile,9,Modem,4,News,9,News & Magazine,1,Nonprofit,1,Operating Systems,3,Personal,1,Personal Blogger Template,1,Phones & Tablets,8,Plugins,3,Premium Blogger Template,5,Responsive blogger templates,4,Review,2,Root,2,Samsung,1,Security,1,Seebait,1,Seo,3,Serial key,5,Software,1,Softwares,2,Solutions,3,Sony,2,Tablets,1,Tecno,2,Telegram,1,ThemeForest,9,Tigo,1,Top 10,1,Tricks,7,Tricks And Tips,13,Tutorial,41,Ubuntu,2,Unlock,3,Utilities,1,Video,1,Videos,1,Vodacom,1,Webdesigns,1,Whatsapp,14,Window7,2,Window8,1,Windows,4,Windows 10,2,Windows 7,3,Windows 8,2,Windows 8.1,1,WordPress Themes,7,WordPress Tutorials,1,Youtube,3,
ltr
item
TRICKS ZOTE: JINSI YA KUBURN UBUNTU AU WINDOWS KWENYE FLASH DISK
JINSI YA KUBURN UBUNTU AU WINDOWS KWENYE FLASH DISK
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEip-1oGe781RzW6qxmBEu7ObF0uBnrIa_z5BZc9E-kIIBzOwpxxHkuow1x_WohPZJk-zm2loGIyF2Kc17NlPh-6CCHWnutcvQQaNTWK9aP7FhBAVOrfCYpTczsc6X_O3o0DX3EfMw-x38U/s1600/create-usb-ubuntu-1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEip-1oGe781RzW6qxmBEu7ObF0uBnrIa_z5BZc9E-kIIBzOwpxxHkuow1x_WohPZJk-zm2loGIyF2Kc17NlPh-6CCHWnutcvQQaNTWK9aP7FhBAVOrfCYpTczsc6X_O3o0DX3EfMw-x38U/s72-c/create-usb-ubuntu-1.png
TRICKS ZOTE
http://zotekalitricks.blogspot.com/2016/12/jinsi-ya-kuburn-ubuntu-au-windows.html
http://zotekalitricks.blogspot.com/
http://zotekalitricks.blogspot.com/
http://zotekalitricks.blogspot.com/2016/12/jinsi-ya-kuburn-ubuntu-au-windows.html
true
1497846088060985027
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy