Habari ndugu wasomaji wa blog hii natumai ni wazima nami pia namzukuru mola wangu kwa kunijaalia kukusogezea haya machache ninayoyafahamu. k...
Habari ndugu wasomaji wa blog hii natumai ni wazima nami pia namzukuru mola wangu kwa kunijaalia kukusogezea haya machache ninayoyafahamu.
kutokana na maisha tunayoishi au ninayoishi nimekutana na tatizo kama hili zaidi ya mara moja mtu kusahau Patten au Password hivyo nikaonelea niwafahamishe nanyi kwani nimeshalipatia ufumbuzi wengi hudhania labda lazima uende kuflash simu yako ndio mambo yaende sawa sasa leo tuachane na kuflash kwa tatizo letu hili
Fuata hatua hizi ili kukamilisha lengo letu

- Zima simu yako toa betri na ulirudishe
- Kama unatumia HUAWEI,VODAFONE AU TECNO bonyeza batani ya kuongezea sauti na ya kuwashia kwa pamoja kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
- kama unatumia Samsung bonyeza batani ya kuwashia, kuongezea sauti na home button kwa sekunde 15, kufanya hivyo kutakuletea Recovery menu.
- 3. Tumia batani ya kupunguzia sauti na ushuke mpaka kwenye wipe data/factory reset
- 4. Bonyeza batani ya kuwashia kisha tumia batani ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data then bonyeza batani ya kuwashia. (kwa baadhi ya simu za tecno na Sony Bonyeza batani ya kuongezea sauti kisha tumia batani ya kupunguzia sauti kushuka mpaka kwenye delete all users data then bonyeza batani ya kuongezea sauti)
- 5. Iache kwa muda kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza batani ya kuwashia kisha iache izime na iwake( kwa baadhi ya simu zitakuomba ukubali kufuta bonyeza batani ya kuwashia kisha utaona neno Reboot now liko highlighted bonyeza batani ya kuwashia kisha iache izime na iwake) kwa kesi ya baadhi ya simu utatumia batani ya kuongezea sauti badala ya batani ya kuwashia.
- 6. Hapo utakuwa umefanikiwa kuondoa pattern au password kwenye simu yako
COMMENTS